Mahakama ya Pakistan mnamo Septemba 30 ilikataa ombi la dhamana la Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan na mkewe Bushra Bibi, katika kesi ya ufisadi, alisema wakili wao.
Ni pigo jingine kwa kiongozi huyo maarufu wa upinzani, ambaye amekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia kwa makosa mengi.
Khan amekumbwa na visa zaidi ya 150 tangu mwaka 2022, alipoondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye bungeni baada ya washirika kadhaa wa kisiasa kumwacha.
Amelishutumu jeshi na adui wake mkuu na Waziri Mkuu wa sasa Shehbaz Sharif kwa kumuondoa madarakani chini ya njama ya Marekani, mashtaka ambayo wameyakanusha.