Michezo

Maisha popote, Enzo Zidane kasajiliwa Morocco

on

Enzo Zidane mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani na Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesajiliwa na club ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Taarifa za kusaini Enzo ndani ya club ya Wydad Casablanca zimetolewa na wakala wale ambaye ni rafiki wa baba yake na mchezaji wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Roberto.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Enzo Zidane amekuwa na wakati mgumu katika soka licha ya kukulia katika academy ya Real Madrid na kudumu kwa miaka 10 lakinj hakupata nafasi ya kucheza timu ya wakubwa na hata alipohamia Alavez hakudumu zaidi ya mwaka na sasa ameondoka timu ya daraja la pili Hispania Almeria na kwenda Wydad.

Soma na hizi

Tupia Comments