Michezo

Hizi ni sababu za Justice Majabvi wa Simba kukataa kuchezea taifa lake…(+Audio)

on

Kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe ambaye ametua Simba msimu huu akitokea klabu ya Vicem Hai Phong F.C ya Vietnam Justice Majabvi ambayo alikuwa amemaliza mkataba wake katika klabu hiyo. Bado anaendelea kukupa ile exclusive interview  aliyofanya na millardayo.com.

IMG-20150826-WA0004

Majabvi akichuana na Ivan Rakitic wa FC Barcelona wakati wote wakicheza Australia Bundesliga

Majabvi amesajiliwa na Simba kwa kiwango kizuri alichokionyesha baada ya kufanya majaribio na klabu hiyo ila swali lilikuwa hivi mbona Majabvi ana kiwango kizuri ila rekodi zinaonesha mara ya mwisho kucheza katika timu ya taifa ya Zimbabwe ni mwaka 2012, tatizo nini?

IMG-20150826-WA0015

“Ndio niliacha kuchezea timu ya taifa kwa sababu ya matatizo mengi katika timu ya taifa, nimecheza timu ya taifa toka mwaka 2004 hadi 2012, kwa sababu ya matatizo binafsi na shirikisho la soka la Zimbabwe, nilikuwa natumia hela yangu kama nauli kuja kucheza timu ya taifa lakini sikuwa nikirudishiwa” >>> Majabvi

Hii ni sauti ya Justice Majabvi

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments