Israel inasema kuwa majadiliano ya ubadilishanaji wa mateka na kundi la Hamas yamefikia kikomo, hii ni mara baada ya Jenerali Nitzan Alon akitoa taarifa hiyo kwa familia za Wana-Israel waliotekwa nyara katika Gaza.
Alon Aliongeza kuziambia familia hizo siku ya Jumanne na kusema kuwa mazungumzo yamekwama, akieleza kuwa “katika wakati huu, hakuna makubaliano
Aidha Familia hizo zilihoji kuhusu muda wa makubaliano, lakini Alon alikataa kutoa tarehe yoyote, jambo lililosababisha kuchochea hasira miongoni mwao, Wawakilishi wa familia hizo walielezea kukata tamaa, wakisema kuwa bila muda maalum, hali inaweza kudumu kwa miezi kadhaa, hasa wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Rais wa Marekani.
Habari kutoka kwa mtangazaji mmoja wa umma wa Israel, zinasema kuwa Tel Aviv imewasilisha pendekezo jipya kwa Washington ili kurahisisha ubadilishanaji wa mateka na kumaliza mzozo wa Gaza kabisa, Hata hivyo, Hamas inasisitiza kuwa haina nia ya kujadili mapendekezo mapya, badala yake inashikilia muundo uliowasilishwa na Rais wa Marekani Joe Biden mwishoni mwa Mei.
Mpango huo unajumuisha kusitishwa kwa mapigano, ubadilishanaji wa mateka na wafungwa, pamoja na ujenzi upya wa Gaza.
Pendekezo jipya la Tel Aviv linaripotiwa kujumuisha “kupatiwa usalama kwa (kiongozi wa Hamas) Yahya Sinwar na wengine wanaotaka kutoka Gaza, kutolewa kwa idadi isiyojulikana ya wafungwa wa Kipalestina, kukabidhi silaha za Gaza, na kutekeleza utaratibu wa uongozi wa eneo hilo.”