Michezo

Matokeo ya Majimaji FC Vs The Might Elephant FC yapo hapa (Audio&Picha)

on

Klabu ya soka ya Majimaji FC  ya Ruvuma Songea bado inazidi kujiandaa kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania bara itakayoanza Septemba 12 kwa michezo kadhaa kuchezwa. Majimaji FC inayofundishwa na kocha raia kutoka Finland Mika Lonnstorm August 26 imecheza mechi ya kirafiki kama sehemu ya maandalizi yake.

IMG_0024 - Copy

IMG_0044

Kocha mkuu wa Majimaji FC Mika Lonnstorm

Majimaji FC  ya Songea imecheza mechi ya kirafiki na timu ya jeshi inayoshiriki Ligi daraja la pili ya The Might Elephant FC na kuibuka na ushindi wa goli 1-0 goli lililofungwa na Peter Mapunda katika dakika ya 15 ya mchezo.

“Tumeweza kuona kile kitu ambacho tunakielekeza kinaenda  vizuri, tutacheza mechi ya combine ya Songea tumeomba iundwe timu itakayojumuisha wachezaji wazuri wote wa Songea na kucheza mechi ya kirafiki ila kama mambo hayataenda vizuri tutasafiri au tutacheza mechi nyingine ya kirafiki ndani ya Songea” >>>Hassan Banyai

IMG_0047

Aliyesimama ni kocha wa The Might Elephant

IMG_0046

IMG_0043

IMG_0015 - Copy - Copy

 Hii ni sauti ya Hassan Banyai kocha msaidizi wa Majimaji FC 

 PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments