Michezo

Kauli ya Azam FC kuhusu mchezaji wao Brian Majwega kuomba kufanya mazoezi na Simba (+Audio)

on

November 18 uongozi wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba ulitoa Press release kuhusu kiungo wa kimataifa wa Uganda anayekipiga katika klabu ya Azam FC Brian Majwega kuomba kujiunga kufanya mazoezi na Simba wakati huu wa Ligi, kitu ambacho kimeshangaza wengi kwa nini aombe kufanya mazoezi na Simba wakati ni mchezaji wa Azam FC na klabu ya Azam FC inaanza mazoezi Jumatatu ya November 23.

millardayo.com ilipata nafasi ya kumtafuta afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga na kuomba kufahamu kuhusu maamuzi hayo ya Majwega au wamemtoa kwa mkopo katika klabu ya Simba na hawajataka kuweka wazi, mkataba wake umemalizika? kuna tatizo gani kati ya Majwega na Azam FC.

majwega

Brian Majwega wa Azam FC kulia akijaribu kumtoka Juma Abdul wa Yanga

” Majwega hatujampeleka klabu yoyote kwa mkopo ila ametoroka kambini na kwenda kwao Uganda lakini  Uganda hawezi kucheza klabu yoyote kwa sababu ana mkataba na Azam FC hivyo hawezi kucheza klabu yoyote, kuhusu kufanya mazoezi na Simba hatuwezi kuzungumzia hatujui wameongea nini ila licha ya kutoroka Azam FC haikumchukulia hatu yoyote ila kwa anachokifanya sasa anahitaji apate adhabu” >>> Jafari Iddi

Hii ni sauti ya Jafari Iddi

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments