SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema makali ya mgawo wa umeme yanaendelea kupungua, baada ya megawati 350 Zilizopunqua siku za hivi karibuni kuanza kureiea na wiki ijayo zitaendelea kushuka hadi megawati 100.
Aidha, limesema hadi Februari mwaka huu hakutakuwa na mgawo wowote kutokana na kituo cha kuzalisha meme cha Kinyerezi | kuongeza upatikanaji wa nishati hiyo kwa uhakika zaidi.
Shirika hilo lilitoa ahadi hiyo katika mahalo wa mtandaoni kupitia Twiter uliouandaa na kushirikisha wananchi ambao wamewataka wanasiasa kukaa kando na kuwaacha watendaji kufanyakazi zao kitaalamu, ili kuwa na suluhisho la kudumu la matatizo ya umeme nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande, wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia mahalo huo wa kumekucha, uliojumuisha zaidi ya watu 1,000 alitoa nafasi ya watu kuuliza maswali na kujibiwa papo hapo.
Alisema TANESCO itaendelea kusema ukweli na kutatua kero za wananchi kwa wakati bila kujali mazingira kwa kuwa lengo ni huduma nzuri, yenye kuridhisha na tia kwa nchi.