Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha zinatoa tenda ya Usafi kwa Kampuni zenye sifa na Vifaa vya uhakika na sio kutoa tenda hiyo kwa Kampuni hewa au kwa kujuana jambo linalopelekea Usafi kusuasua.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa zoezi la Usafi wa pamoja Kata ya Kariakoo kwa ushirikiano na Kampuni ya Usafi ya Kajenjere trading company.
Aidha RC Makalla amewataka Wakandarasi wa Usafi kuhakikisha wanabeba taka kwa wakati na kuwahimiza Wananchi kulipa ada ya taka.
Pamoja na hayo RC Makalla amewapongeza Wananchi kwa kuhamasika kufanya Usafi Jambo lililopelekea Dar es salaam kushika nafasi ya sita kwa Usafi barani afrika na kuwa miongoni mwa.majiji mawili yanayovutia barani afrika.
Hata hivyo RC Makalla amesema Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM ni Kampeni endelevu hivyo ameelekeza kila Mtaa kuhakikisha wanadhibiti Ufanyaji biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa.