Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) Septemba 22, 2021 ilitangaza Club 20 za soka Tanzania ambazo zimeingiza Mashabiki wengi viwanjani (home ground) katika msimu wa 2020/2021.
1- Yanga SC Mashabiki 141,681
2- Simba SC Mashabiki 138,518
3- Dodoma Jiji FC Mashabiki 27,455
4- JKT Tanzania Mashabiki 25,062
5- Mwadui FC Mashabiki 22, 232
Hizi ni baadhi tu ila orodha iliyotangazwa inafikia Club 20.
Kwa upande wa mapato Bodi ya Ligi kuu Tanzania Bara (TPLB) ikataja Club za soka zilizopata mapato mengi kupitia viingilio vya mlangoni kwa msimu mzima wa 2020/2021
1- Yanga SC Tsh millioni 986.8
2- Simba SC Tsh milioni 929.7
3- JKT Tanzania Tsh milioni 148.1
4- Dodoma jiji Tsh milioni 139.3
5- Ihefu FC Tsh milioni 138.6
Hizi ni baadhi tu ila orodha iliyotangazwa inafikia Club 20. Sasa kinachoendelea mitandaoni kwasasa ni watu mbalimbali wakiendelea kuhoji juu ya takwimu hizo zilizotolewa hapa nimekusogezea alichokisema Waziri wa Nishati January Makamba kisha kujibiwa na Msemaji wa Yanga SC Haji Manara
MANARA AFUNGUKA BAADA YA KUTANGAZWA KWA TAKWIMU ZA BODI YA LIGI KUU TANZANIA BARA