Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amekasirishwa na kitendo cha mtu mmoja kuweka mikono mfukoni wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Dkt. Mpango ameyasema hayo Mkoani Morogoro katika hafla ya kuikabidhi TANAPA malori 44 yenye thamani ya Bilioni14.7 kutoka mradi mradi wa Kuboresha Maliasili na Kukuza Utalii
Kusini (REGROW).
“Huo sio utaratibu na heshima kwa Wimbo wa Taifa letu, nawasisitiza tuzingatie utaratibu na heshima inayostahili kwa tunu hii kubwa ya Taifa letu, wimbo Taifa ndio unatutambulisha” Makamu wa Rais.