Makamu wa Rais wa Marekani jana aliwasili nchini Ghana kuianza ziara taje ya wiki moja barani Afrika na katika hotuba yake jana alisema kuwa, Marekani itazidisha uwekezaji wake barani Afrika na kusaidia kuchochea ukuaji wa uchumi pia ziara hii inalenga kukabiliana na ushawishi wa nchi hasimu ya China.
Serikali ya Rais wa Marekani Joe Biden inadai kuwa inataka kuimarisha uhusiano na Afrika, kama njia mbadala ya kukabiliana na ushawishi wa mahasimu wa Washington barani Afrika. Mwezi Desemba mwaka jana, kabla ya mkutano wa kilele wa Marekani na Afrika, Washington ilitoa dola bilioni 55 kwa bara la Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Harris Kamala wiki hii atakuwa na mazungumzo na Rais Nana Akufo- Ado wiki hii na atatembelea na gome ya zamani ambayo watumwa walisafrishwa hadi Amerika wakati wa enzi ya biashara ya utumwa.
Kamala Harris jana aliwasili ziarani huko Ghana ambapo atasalia hadi tarehe 29 mwezi huu wa Machi, kisha atakuwa Tanzania kuanzia Machi 29-31. Aidha atakuwa ziarani Zambia, kuanzia Machi 31 na Aprili 1.
Makamu wa Rais wa Marekani atakutana na Marais wa nchi hizo tatu na anapanga kutangaza uwekezaji wa nchi yake katika sekta za umma na binafsi katika nchi hizo tatu.
Itakumbukwa kuwa, China imefanya uwezekaji mkubwa barani Afrika katika miongo ya karibuni ikiwa ni pamoja na kuwekeza vitega uchumi katika miundombinu na kukuza rasilimali huku ushawishi wa Russia ukiongezeka barani Afrika kupitia masuala mbalimbali kama kutuma wanajeshi kutoka kwa mkandarasi binafsi wa kijeshi wa Kampuni ya Wagner Group ya nchi hiyo ili kuzisaidia serikali mbalimbali barani Afrika.