Makamu wa rais wa zamani wa Marekani, Mike Pence, atazindua kampeni yake ambayo ilikuwa ikitarajiwa ya kuwania uteuzi wa chama cha Republikan kugombania urais wiki ijayo jimboni Iowa.
Kutokana na hili amekuwa mgombea mwingine katika uwanja mpana wa ugombea urais wa Republikan, na kumfanya awe mpinzani wa bosi wake wa zamani.
Pence atazindua kampeni zake mjini Des Moines Juni 7, ambayo ni tarehe yake ya kuzaliwa akifikisha miaka 64 kwa mujibu wa watu wawili wanaofahamu mipango yake ambao hawakutaka kutambuliswa.
Washirika wa Pence walisema mapema mwezi huu kwamba PAC kuu iliyozinduliwa ili kumuunga mkono mgombeaji wake, Committed to America, itaandaa katika kaunti zote 99 za Iowa. Vyanzo vilisema wakati huo kutarajia Pence kutumia wakati zaidi katika Jimbo la Hawkeye katika miezi ijayo.
Kabla ya kutajwa kuwa makamu wa rais wa Trump katika uchaguzi wa 2016, Pence alikuwa gavana wa Indiana na mbunge wa zamani wa Marekani, ikiwa ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Baraza la Republican.
Pence na Trump walikuwa na mzozo baada ya Trump kumshinikiza Pence kuzuia uidhinishaji wa matokeo ya uchaguzi wa 2020 na uasi katika Ikulu ya Marekani mnamo Januari 6, 2021, ulihatarisha Pence na familia yake.
Pence atajiunga na kundi linalokua la Warepublican wanaotaka kuchukua mikoba ya Rais Joe Biden, ambaye anawania muhula wa pili pamoja na Trump na DeSantis, balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Nikki Haley, Seneta wa Marekani Tim Scott, Gavana wa zamani Asa Hutchinson, na mjasiriamali Vivek Ramaswamy pia wanawania uteuzi wa GOP.