Habari za Mastaa

Hizi ndizo sababu zilizomfanya Makamua kuwa kimya.

By

on

makamuaaaMakamua,Q jay na Joselin waliwahi kuwa pamoja kikazi na kundi lao la Wakali kwanza ambapo baadae  zilitoka taarifa za kuokoka kwa Q jay na kuachana na muziki,japo kuna taarifa ambazo si rasmi zimetoka kwamba Q jay kwa sasa ameanza kuandaa nyimbo za Gospel so watu wajiandae kumpokea upande huo.

Millardayo.com imeongea na Makamua kuhusu kuwa kimya kimuziki na hiki ndicho alichokisema>>’Binafsi  nina track zaidi ya 58 ambazo sijaziachia,bado kuna project nyingi nimefanya sehemu mbali mbali kama Legenday,Fundi Samwel na Mona Gangstar’  ambazo naaziandaa kuwepo kwenye album yangu ya Beautiful Melody.

‘Nategemea kuachia video ya ngoma mpya inaitwa ‘She is Gone’ halafu kuna ujio mwingine upande wa audio japo sijajua ngoma gani nitaachia maana ziko nyingi nimeachia ngoma Mission Impossible kwa hiyo nitaachia audio nyingine ambayo nitaifanyia video na kampuni ya Dreamz video’

‘Nina mambo mengi kwa sasa maana nafundisha darasa la muziki,majukumu ya familia pia yananizonga ndiyo sababu nashindwa kuwa kasi kama kipindi cha nyuma,Kwa sasa nimeanza kuingia kwenye tasnia ya movie na mwezi wa tatu naanza kushoot movie inayoitwa Bongo na fleva’.

Makamua ni baba wa watoto wawili na bado mwanafamilia wa Wakali Kwanza  ambayo kwa sasa inaundwa nayeye mwenywe, Joselin  na Kekuu.kwa sasa wanaandaa track yao inayoitwa Nitarudi ambayo wamefanya kwa pamoja.

 

 

Tupia Comments