Ishu kubwa sasa hivi Dar es salaam ni dawa za kulevya ambapo leo February 6 2017 Kamishna wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amezungumza na Waandishi wa habari na kutoa takwimu ya kilichofanyika ndani ya siku 3.
“Tunaendelea vizuri na Oparesheni yatu ya kupambana na dawa za kulevya, tumekamata jumla ya Watuhumiwa 112 na jumla kete 299 zidhaniwazo kuwa ni dawa za kulevya, kwa kawaida tutazipeleka kwa mkemia mkuu wa Serikali na atatuambia ni aina gani”
“Katika Watuhumiwa hao 112, 12 tumewapeleka leo Mahakamani sababu sheria ya mwenendo wa mashtaka iko wazi, huwa inaturuhusu kuomba kuwaombea Watuhumiwa kwa kiapo kwa Hakimu, wawe chini ya uangaliazi wa Jeshi la polisi na Mahakama kwa muda wa miaka miwili wasifanye makosa tena‘
“Wote tuliowakamata wengine wanakiri na wamekwenda kuonyesha hizo dawa za kulevya, kusudio la kwanza ni wawe chini ya uangalizi wetu na kusudio la pili la kiapo chetu ni waache hiyo tabia wawe raia wema, kusudio la tatu wawe wanakuja kuripoti kituo cha polisi angalau mara mbili kwa mwezi…. lengo letu ni kuona je wameacha kutumia dawa za kulevya?” – Kamishna Simon Sirro
POLISI MAKAO MAKUU KANDA DSM https://t.co/tP6VyMuRtJ
— millardayo (@millardayo) February 6, 2017
FULL VIDEO: Paul Makonda kuhusu kilichoendelea na kinachofatia kuhusu dawa za kulevya, tazama kwenye hii video hapa chini
VIDEO: Wema Sepetu, T.I.D na wengine walivyoingia Polisi kutii wito wa Paul Makonda