AyoTV

Video ya Dc Makonda alivyotangaza kuwawajibisha waliohusika na uharibifu wa barabara za Kinondoni

on

Siku ya March 11 2016 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alifanya ziara ya kutembelea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya yake na kushuhudia kero za uharibifu wa miundombinu ikiwepo barabara na kuamua kutoa agizo kwa Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha inafanya ukarabati huo ndani ya siku 14 kabla ya kuwawajibisha.

Makonda amesema ‘Nimejionea ubovu wa barabara za Kinondoni, lakini hii si’mara ya kwanza, mara ya kwanza niliona ubovu huu na nikaunda kamati ya wataalam wakachunguza na kubaini barabara nyingi zilijengwa chini ya kiwango

Hatua hii ilipelekea kusimamishwa kwa baadhi ya watumishi, lakini cha ajabu barabara zinazidi kuwa mbovu na wananchi wanalipa kodi, nimejionea pale Hospitali ya Mwananyamala mama mmoja akijifungulia kwenye bajaji, mbaya zaidi juzi kuna ajali imetokea na mtu akafa

Nini maamuzi yake baada ya haya yote? ‘Sasa nimeiagiza Manispaa, nimewapa wiki mbili kuhakikisha mashimo yote yawe yamezibwa, na wakishindwa nitawasaidia kuwawajibisha na kuchukua hatua stahikiPaul Makonda

Hapa unaweza kuitazama Full video ilivyokuwa…..

Ilikupita hii Video ya Siku moja kabla ya Walimu kuanza kusafiri bure, Dc Makonda kachukizwa na haya maneno?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments