Top Stories

Makontena 187 ya vinia yaruhusiwa kwenda nje ya nchi

on

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ameruhusu kusafirishwa kwa makontena 187 ya Vinia kwenda nchi za nje  yaliyokuwa yamezuiwa katika  bandari ya Dar es Salaam kuanzia tarehe 15 Novemba  , 2021 kufuatia tamko la Serikali la kuzuia usafirishaji wa malighafi za mazao ya misitu kwenda nje ya nchi.

Dkt. Ndumbaro ametoa ruhusa hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na  Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wakati wa mkutano ulioitishwa na Wafanyabiashara hao kupitia Baraza la Taifa la Wafanyabishara (TNBC).

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia ombi la Wafanyabishara wa mazao ya misitu kutaka waongezewe muda wa kusafirisha mazao hayo yaliyokuwa  bandarini ambayo yalizuiliwa kufuatia tamko alilolitoa Novemba 15 mwaka huu.

Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa ruhusa hiyo inayahusu  makontena 187 yaliyokuwa bandarini na si vinginevyo akisisitiza kwamba msimamo wa Serikali wa kutoruhusu uvunaji na biashara ya gundi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania uko pale pale hadi watafiti watakapotoa majibu juu ya hasara na faida yake.

”Naomba nieleweke vizuri ruhusa hii ya kusafirisha vinia itahusu makotena 187 tu ambayo nyaraka zake tayari zilishawasilishwa kwenye vyombo vya kiserikali” Dkt. Ndumbaro.

Katika hatua nyingine, Serikali imewaongezea muda Wafanyabiashara wa mazao ya misitu nchini kusafirisha vinia kuanzia leo hadi tarehe 30 Juni 2022 kwa  kuzingatia vigezo na masharti yaliyoweka.

Ameyataja masharti hayo kwa wafanyabiashara hao  kuwa ni kutakiwa kuwasilisha mpango kazi  wa kuleta mashine ya kuchakata vinia hadi hatua za mwisho pamoja na kuwasilisha taarifa za kodi na malipo mengine ya serikali

Mbali na masharti hayo, Dkt. Ndumbaro  amesema wafanyabiashara hao ili waweze kuruhusiwa kusafirisha mazao hayo watatakiwa kuwasilisha  taarifa za haki za Wafanyakazi katika viwanda vyao pamoja na gharama halisi za mzigo husika.

INAHUZUNISHA MZEE ALIYEJIKATA NYETI ZAKE ILI AFE “MKE KANIKIMBIA, BUNDUKI INASHTUKA”

Tupia Comments