Kabla ya kufungwa kwa dirisha la uombaji mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini baadhi ya makosa yamebainika kufanywa na baadhi ya Waombaji hali inayowaweka kwenye hatari ya kupoteza fursa ya kupata mkopo.
Dirisha la Mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 lilifunguliwa June 1, 2024 likitarajiwa kutoa mikopo kiasi cha Shilingi bilioni 787 kimetengwa kwa ajili ya mikopo hiyo.
Baadhi ya makosa yaliyobainika ni kutokamilisha taarifa muhimu zinazotakiwa katika utumaji wa maombi hayo huku
ikibainika kuna wazazi wanaojaza fomu za maombi ya mikopo kwa niaba ya waombaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania, Dk Bill Kiwia amewataka wazazi kuacha kuwajazia fomu za maombi watoto wao kwa kile alichoeleza wengi wao hawana taarifa muhimu zinazohitajika hivyo kusababisha maombi kutokamilika.