Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, UN Antonio Guterres amefurahishwa na tangazo la jana Jumatano la makubaliano ya usitishaji vita huko Gaza na uachiliwaji wa mateka. Lakini amesisitiza, “Kipaumbele chetu lazima kiwe kupunguza mateso makubwa yaliyosababishwa na mzozo huu.”
Guterres amezitaka pande zote kutii kikamilifu makubaliano hayo. Amesema, “Ni muhimu kuwa usitishaji huu wa vita uondoe vikwazo vyote vya kiusalama na kisiasa ili kupeleka msaada kote Gaza.”
Katibu mkuu huyo ameyaita makubaliano hayo “hatua muhimu ya kwanza.” Lakini amesema kumaliza “utwaaji wa maeneo na kufanikisha suluhu iliyojadiliwa ya mataifa mawili, na Israel na Palestina kuishi pamoja kwa amani na Usalama,” bado ni vipaumbele vya dharura.