Taifa la kusini mashariki mwa Afrika la Malawi limetangaza hali ya maafa katika wilaya 23 kati ya 28 za nchi hiyo zilizoathiriwa vibaya na vipindi vya ukame vinavyosababishwa na El Nino na mafuriko “ili kuruhusu msaada wa kibinadamu kuingia na kudhibiti hali hiyo.”
Katika hotuba yake kwa taifa Jumamosi jioni, Rais Lazarus Chakwera alisema: “Tathmini yetu ya awali inaonesha kuwa kaya milioni 2 za wakulima zimeathirika na hekta 700,000 za mahindi (ambayo ni zao kuu la kaunti) zimeharibiwa ikiwa ni asilimia 44 ya mazao ya kitaifa. ”
Serikali ya Malawi pia iliomba mwitikio wa haraka wa kibinadamu kutoka kwa washirika wake wa maendeleo na wananchi wa ndani na nje ya nchi ili kuepusha mzozo wa kibinadamu ambao umeweka takriban kaya milioni mbili za wakulima katika hatari ya njaa.
“Wilaya hizi zimekuwa na mvua za kusuasua, mafuriko na ukame wa muda mrefu ambao umeharibu sana mazao na matarajio ya uzalishaji wa chakula,” Chakwera alibainisha.