Top Stories

Mama ajifungua Watoto watano kwa mpigo Mbeya (+video)

on

Binti mmoja mkazi wa Kata ya Mwakibeta Jijini Mbeya ajulikanaye kwa jina la Emelia Joram (21), amejifungua watoto watano katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Mbeya huku mmoja kati yao akiwa amekufa.

Binti huyo alijifungua Oktoba 31 mwaka huu kwa upasuaji ambapo watatu kati yao ni wa kike na mmoja pekee ndiye wa kiume na wawili wapo kwenye chumba cha joto kutokana na kuzaliwa wakiwa na uzito pungufu.

Kutokana na hali hiyo wadau mbalimbali wameombwa kumsaidia kumsaidia mama huyo kwenye malezi ya watoto hao ili wakuwe katika hali nzuri.

WAZIRI MKUU AULIZWA KUHUSU MALALAMIKO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, ATOA KAULI

Soma na hizi

Tupia Comments