Top Stories

Mama akiri kuua Watoto wake wanne Kenya

on

Mwanamke mmoja nchini Kenya Betrice Mwende, anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne, amekiri Mahakamani kuwa ni kweli alifanya tukio hilo na alilitekeleza kwa kumnyonga mmoja baada ya mwingine na kwamba alikuwa anajisikia vizuri mno wakati anatenda unyama huo.

Betrice Mwende mwenye umri wa miaka 41, ambaye pia ni Mwalimu wa Hisabati, amekiri tuhuma hizo mbele ya Hakimu Mkaazi wa Mahakama ya Naivasha Yusufu Barasa, na kusema kuwa alianza kumuua kwa kumnyonga mwanaye mdogo mwenye umri wa miaka miwili Whitney Nyambura na kisha kuwaua wengine Melody Warigia (8), Willy Macharia (6) na Samantha Njeri (4)

Mwende amedai kuwa alitekeleza unyama huo kutokana na msukumo wa nguvu asizozielewa, huku akimlaumu mmewe walioachana kwa kusababisha maafa ya wanawe.

Kwa upande wa Mahakama ya Naivasha metoa siku saba zaidi za mwanamke huyo kuzuiliwa ili aweze kufanyiwa uchunguzi wa akili, na mwanamke huyo amemwomba kaka yake kumsaidia kuwazika wanawe, huku akiiomba Mahakama kumsamehe kwani hakuelewa alichokuwa akifanya.

“WAFUKUZENI KAZI HAWAFAI WANATOZA HELA KUBWA” BASHUNGWA AAGIZA KWA SIMU

Soma na hizi

Tupia Comments