Top Stories

Mama aliewaua watoto wake kwa sumu afunguka “maisha magumu tunalala njaa” (+video)

on

Mwanamke aitwae Veronica Gabriel (30) wa Chato, Geita ambaye anatuhumiwa kuwaua kwa sumu Watoto wake wawili kati ya watano amehojiwa akiwa chini ya ulinzi wa Polisi na kuendelea kusisitiza kuwa ugumu wa maisha ndio chanzo cha yeye akawaua Watoto wake huku ikielezwa kwamba aliwanywesha wote na yeye kunywa lakini waliofariki ni wawili.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule akiambatana na Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wa Geita alifika kwenye kituo cha Bwanga na kuzungumza na Mtuhumiwa huyu.

“Sio kusudi langu ila ndio maisha yamenipiga kwakweli nilikuwa sina ramani yoyote ile maisha ndio yaliyonipiga wakati mwingine mnalala nje na mnashinda na njaa vibarua hadi unachoka hata nguvu zinaisha wakati mwingine nikaona bora nife, Ndugu zangu walishanitenga, nina Kaka watatu wameshanitenga nikaona hata nikiwaacha Watoto watateseka tu nikaona bora nife nao”

Soma na hizi

Tupia Comments