Wakati Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro likiwa linamtafuta Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani anayetuhumiwa kumpa ujauzito Mtoto wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 14 ambaye inasemekana ni mtoto wa Polisi mwenzake, Mama wa mtoto ameongea nakusema hata simu aliyokuwa anatumia Mtoto huyo alinunuliwa na Askari huyo
Mama wa mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa anasema aligundua baada ya kumkuta na simu nakuangalia picha kwenye mtandao wa WhatsApp nakubaini hilo na alipomuuliza Mke wa mwanaume huyo alidai kwamba analifahamu hilo suala na alishamuonya Mume wake.