Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Vijana wa Jamii ya wafugaji wa kabila la Wasukuma kuwalazimisha Wanawake Kwa nguvu kufanya nao mapenzi na kutaka kuwaoa bila ridhaa yao, DC Ngollo amesema mila hizo maarufu kwa jina la Chagulaga zimepitwa na wakati.
Kauli hiyo ameitoa akiwa katika Kijiji Cha Igumbiro katika mwendelezo wa ziara yake ya kusikiliza kero za Wananchi katika Vijiji vya Wilaya hiyo, jambo hilo liliibuka baada ya Wanawake kutoa malalamiko yao Kwa DC Ngollo akiwa Kijijini hapo na kusema kuna baadhi ya Wanaume wanalazimisha Wanawake kufanya nao mapenzi ama kuwaoa bila ridhaa yao na hufanya hivyo kwa kuwavizia Wanawake wakiwa wanaenda shambani au wakiwa kwenye minada.
Wananchi wanasema Wanaume hao wakikutana na Wanawake humzunguka na kumwambia achague Mtu mmoja afanye nae mapenzi na akikataa analazimishwa “Mwanamke akikataa anapigwa viboko kama kuna Baba yako au Bwana wako akija anapigwa viboko na yeye”