Top Stories

Mama Mlemavu aliechangiwa pesa ya Bajaji na hayati Magufuli aibiwa bajaji (video+)

on

Nyangoma James ni Mlemavu ambaye Hayati Magufuli alimchangia Mil 5 Ubungo Dar es salaam na akachangisha Watu wengine hadi ikapatikana zaidi ya Tsh. Milion 8 ambayo Nyangoma alinunua Bajaji na akawa Dereva yeye mwenyewe akiwa anafanyia biashara, lakini Jumamosi Wiki hii Bajaji yake imeibwa nyumbani alikopanga Kibaha, Mkoani Pwani.

Licha ya kuwa na Watoto watatu ambao wawili anawasomesha kwa sasa, Nyangoma pia anaishi na Baba yake Mzazi ambaye amepooza miguu na ile Bajaji aliyoinunua kwa msaada wa Hayati Magufuli ndio ilimwezesha kuwahudumia Watoto na Baba yake, namba za kumsaidia 0758311341 (imesajiliwa kwa jina la Joyce Songora).

EXCLUSIVE: WAFUNGA NDOA WODINI BAADA YA MUME KUPATA AJALI NA KUKATWA MGUU NA VIDOLE, WOTE WAFUNGUKA

Soma na hizi

Tupia Comments