Michezo

Mama mzazi wa Mbappe aikataa Madrid

on

Mama mzazi wa mshambulia Kylian Mbappe Fayza Lamari amesema hakukuwa na makubaliano yoyote ambayo walifikia na Real Madrid Juu ya uhamisho wa Mbappe kujiunga na klabu hiyo.

Mbappe amekuwa akihusishwa kujiunga na Real Madrid lakini mapema hii leo imeripotiwa kuwa atasaini mkataba mpya wa kusalia PSG. Mkataba wake wa sasa na PSG unamalizika June 30 2022.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Tweeter Mama wa mshambuliaji huyo ambaye anamsimamia mtoto wake alimjibu mwandishi wa habari za michezo wa Ufaransa Frederic Hermel ambae aliandika kupitia mtandao huo kuwa Mbappe anapaswa kuheshimu makubaliano aliyoingia na Madrid. Ndipo Fayza akamjibu,

“Bwana Hermel, kama hatujui kitu, huwa tunanyamaza. Hakukuwa na makubaliano. Zingatia” Ameandika Mama mzazi wa Mbappe

Soma na hizi

Tupia Comments