Top Stories

Mama na mwanae wakamatwa na gunia la dawa za kulevya “watafungwa miaka 30” (+video)

on

Watu watatu wakiwemo wawili wa familia moja, Mama na Mtoto wake wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Wilayani Rombo baada ya kukutwa na gunia saba dawa za kulevya aina ya Bangi ambazo ni sawa na Kilogramu 373 ikisafirishwa kutoka Mkoa wa Arusha kwenda nchi jirani ya Kenya kupitia mpaka wa Holili.

Huu ni muendelezo wa udhibiti wa matukio yanayofanywa na baadhi ya watu mpakani mwa nchi jirani ya Kenya na Tanzania katika Wilaya ya Rombo .

Udhibiti unaosimamiwa kwa karibu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Wilaya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo Dr. Athumani Kihamia pamoja na vyombo vya dola likiwemo Jeshi la Polisi.

Soma na hizi

Tupia Comments