Top Stories

Mama simu aliyonunuliwa na Mumewe yampa ushindi wa gari kutoka Tecno

on

KAMPUNI ya simu za mkononi ya TECNO leo imewakabidhi wateja wake waliojishindia kwenye promosheni ya Vimba na TECNO Camon 17 na TECNO Spark 7 Series kwa kumkabidhi zawadi mbalimbali washindi wa shindano hilo.
Washindi hao wamejinyakulia mshindi gari jipya, huku wengine wakiondoka na mafriji, pikipiki na zawadi mbalimbali.
Hayo yamefanyika leo Agosti 27,2021 kwenye Hafla ya kuwakabidhi washindi hao watano zawadi zao katika ofisi za TECNO zilizopo Jengo la China Plaza kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo Sofia Suleiman ameibuka na gari jipya aina ya Suzuki ambalo halijawahi kutembea hata kilomita moja yaani Zero kilomita.
Wengine waliokabidhiwa zawadi zao ni Marystellah Carlos na Castro Charles waliojishindia friji kila mmoja na mshindi mwingine Juma Kadama yeye aliibuka na pikipiki kubwa aina ya Sunling.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa TECNO Tanzania, William Mota amesema kampuni hiyo ina furaha kubwa kuwakabidhi zawadi hizo wateja walioshiriki promosheni iliyoanza Julai 19 mpaka Septemba 13 mwaka huu ikiwashirikisha wateja wa nchi nzima.
“Leo TECNO tunafuraha kubwa kuwakabidhi zawadi hizi wateja wetu walioshiriki promosheni hii na tunawaomba waendelee kutumia simu za TECNO ambazo ubora wake ni wa hali ya juu.” Amesema Meneja Mota.
Naye Bi. Sofia aliyeibuka mshindi wa gari amesema aliipata bahati hiyo baada ya kununua simu aina ya TECNO Camon 17 na kujikuta akiibuka na zawadi hiyo.
“Jamani mimi nilinunua simu ya TECNO Camon 17 nikiwa sijui kama nitashinda chochote lakini Mungu mkubwa hivi karibuni nikapigiwa simu na watu waliojitambusha kuwa wanatoka TECNO na kuniambia nimeshinda gari.” Amesema Mshindi
Amesema kuwa aikuwa rahisi kuamini kwani alijua ndiyo matapeli lakini walivyozidi kuniweka sawa ikabidi jambo hilo akamshirikisha mume wake ambapo wakaanza kufuatilia maelekezo yao kiundani ndipo wakabaini kuwa ni kweli wamejishindia gari kutoka TECNO.
“Nawaomba TECNO waendelee kuwa wakweli hivihivi kwenye bahati nasibu zao kama walivyonifanyia mimi ambaye hawanijui nami sikuwa nikiwajua zaidi ya kuona bidhaa zao.” Amemaliza Bi. Sofia
Washindi wa promosheni ya Vimba na TECNO Camon 17 na TECNO Spark 7 Series wakiwa katika picha ya pamoja leo mara baada ya kujishindia zawadi mbalimali kutoka kampuni ya Simu za Mkononi ya TECNO.
Meneja Masoko wa TECNO Tanzania, William Mota (kushoto) akimkabidhi funguo ya gari mume wa Bi. Sofia alipokuwa akiwakabidhi gari hiyo. Bi Sofia (mwenye baibui) akishuhudia wakiwa ni amojawapo ya washindi wa promosheni ya Vimba na TECNO Camon 17 na TECNO Spark 7 Series.
Bi. Sofia na mumewe wakiwa ndani ya gari hiyo baada ya kukabidhiwa mara baada ya kujishindia gari katika promosheni ya Vimba na TECNO Camon 17 na TECNO Spark 7 Series .
Afisa wa TECNO, Bella (kushoto) akimkabidhi funguo ya pikipiki mshindi,Juma Kadama baada ya kujishindia kwenye promosheni ya Vimba na TECNO Camon 17 na TECNO Spark 7 Series  leo Agosti, 27, 2021.

Soma na hizi

Tupia Comments