Magazeti

Umesikia mwanamke aliyemnyonga mwanaye wa miaka miwili ili ‘ajirushe’?

on

Screen Shot 2014-11-10 at 1.28.08 PM

Mtoto huyu hausiki na tukio lililotokea.

Wapo Wanawake ambao wamekua wakihangaika usiku na mchana ili waweze kupata watoto lakini wapo wengine ambao wamekua wakipewa watoto hao na Mungu lakini hukufuru kwa kuwaua kwa sababu tu hawana uwezo kifedha kuwalea na wengine kutokua tayari kuitwa mama.

Ni mara ngapi tumeona Wanawake wanatumia picha nzuri za watoto au wanazipost kwenye mitandao ya kijamii wakitamani kuwa nao lakini hawawezi?

Ni kawaida sana kwa sasa kusikia mama kamuua mwanaye aidha kwa kumtupa akiwa hai ama kumuua kabisa ili aweze kupoteza ushahidi na kuendelea na mambo yake.

Huko Sengerema Mwanza mama mmoja Magreth Martini mwenye miaka 20 amenusurika kuuawa na watu wenye hasira baada ya kumnyonga mwanaye wa miaka miwili kisha kumzamisha katika Ziwa Victoria.

Mama huyo anatuhumiwa kuchukua uamuzi huo kwa madai ya mwanaye kumnyima muda wa kujirusha kwa kufanya mambo yake binafsi ambapo wanakijiji waliona mwili wa mtoto huyo ukielea kando kando ya Ziwa hilo huku mama yake huyo akiendelea na huduma kwenye mgahawa wa pembezoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlolowa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa baada ya kuhojiwa na Polisi alikiri kumnyonga na kumzamisha mtoto wake Ziwani.

Mtendaji wa kijiji Charles Subira alisema alifanya juhudi za ziada kuokoa maisha ya mtuhumiwa huyo toka kwa wananchi waliokua na hasira kutaka kulipiza kisasi ambapo walitaka kumuua kisha mwili wake kuuchoma moto.

bby itemsAlisema awali mama wa mtoto huyo alimtelekeza mwanaye kwa jirani na siku moja kabla ya tuko alikwenda na kudai anataka kwenda naye kazini ndipo baadaye mwili wa mtoto huyo ukakutwa unaelea pembezoni mwa Ziwa Victoria.

Gazeti la Nipashe Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Buhama Eliud Bahama  alithibitisha kupokea mwili wa mtoto huyo na kusema kifo chake kimetokana na kunyongwa shingoni.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments