Waziri wa Nishati January Makamba amesema kazi ya kuunganisha mitambo ya kufua umeme kwenye Bwawa wa Mwalimu Nyerere inaendelea ambapo kwa sasa ujenzi huo wa Bwawa kwa ujumla umefika asilimia 85.06.
Na Hapa nimekusogezea mambo matano kuhusu ziara ya Waziri wa Nishati, January Makamba kwenye Bwawa la Nyerere.
1. Ujazo wa maji umefika mita za ujazo BILIONI 6.
2. Kina cha maji kimebakiza urefu wa MITA 13 tu, kufikia kiwango cha kuzungusha mitambo ya kufua umeme.
3. Kazi ya kuunganisha mitambo ya kufua umeme inaendelea.
4. Kwa mvua zilizonyesha maji yameingia mengi kuliko yalioleta mafuriko 2019/20. Tuta la Bwawa hili na kazi ya kujaza maji vimesaidia kuepusha mafuriko Rufiji.
5. Ujenzi wa Bwawa kwa Ujumla Umefikia 85.06%.