Msemaji Mkuu wa serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli imefanikiwa katika utekelezaji wa sera zake katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, afya, miundombinu na uboreshaji wa uwekezaji.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano katika kipindi cha miaka mitano ambapo miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme nchini kutoka megawati 1,308 mwaka 2015 hadi kufikia megawati 1,602.32 mwaka 2020.
“Tume ya Madini imeanza kazi kwa kasi katika kipindi hiki, marekebisho na kutungwa kwa sheria mpya za kusimamia mikataba yenye changamoto na umiliki wa madini vimefanyika na kuleta mageuzi makubwa” Abbasi
“Jumla ya TZS Bilioni 5.2 imelipwa kwa wananchi 618 kati ya 693 watakaopisha mradi katika eneo la Likong’o, Lindi.” Msemaji Mkuu Abbasi
“Serikali ya awamu ya tano pia imetumia takribani TZS Trilioni 1.109 ya fedha za ndani kutekeleza miradi mikubwa miwili ya umeme wa gesi: Kinyerezi-I Extension megawati 185 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 188 sawa na zaidi ya TZS Bilioni 315.4” Msemaji Mkuu Abbasi
“Tume ya Madini imeanza kazi kwa kasi katika kipindi hiki, marekebisho na kutungwa kwa sheria mpya za kusimamia mikataba yenye changamoto na umiliki wa madini vimefanyika na kuleta mageuzi makubwa”Msemaji Mkuu Abbasi
“Kisa cha mchimbaji mdogo Saniniu LaIzer ambaye Juni 24, 2020 aliishangaza Dunia baada ya kuiuzia Serikali Madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 9.27 na kisha akapata jiwe la kilo 5.80 ni ushuhuda wa mafanikio ya ukuta wa Mirerani” Msemaji Mkuu Abbasi