Mix

Mambo ya kufahamu kuhusu Wiki ya huduma kwa wateja UBA

on

KWA kutambua jukumu muhimu linalofanywa na maofisa wa huduma kwa wateja na mawakala wake, Benki ya UBA Tanzania imezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo inatoa fursa kwa benki hiyo kusherehekea pamoja na wateja wao kwa kuthamini kazi ya maofisa wa huduma kwa wateja katika kuhakikisha viwango bora na furaha ya wateja vinazingatiwa na benki hiyo.

Timu ya Utendaji ya UBA Tanzania ikiongozwa na Mkuu wa Kampuni ya Benki ya UBA Tanzania, Mussa Kitambi, walikuwa na tukio la kukata keki na kutoa zawadi kwa wateja na wafanyakazi wao kama alama ya kuthamini na kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani iliyoanza Oktoba 5 hadi 9 mwaka huu.

Kaulimbiu yao inasema ‘Ndoto ya Timu’ ambayo inajumuisha mambo yote ambayo benki inawakilisha ikiwemo maadili yao ya msingi ikiwemo Ubora, Biashara na Utekelezaji ambayo kwa pamoja yanawafanya kushinda kwa pamoja kama timu.

Alisema wiki hiyo ya huduma kwa wateja ni matokeo ya uthabiti wa UBA katika kuimarisha ushirikishaji wa wafanyakazi na hamasa katika kutoa huduma bora kwa wateja. Katika tukio hilo, maofisa wote wa huduma kwa wateja walipongezwa kwa kazi nzuri  na kujituma na kuwajengea imani wateja.

“Lengo letu kuu ni kuonesha falsafa ya kwanza ya C1st kwa mteja kama ‘njia ya maisha’ katika ushirikiano wetu na wateja. Kwa kweli hiki ndiyo kiini chetu na tungetaka kutambulika hivi siku zote, UBA ni taasisi isiyo na shaka katika kutoa huduma bora za kifedha kwa mtazamo wa wateja,”alisema Kitambi.

UBA Tanzania ni benki tanzu ya benki kubwa duniani ambayo inapatikana katika nchi 20 za Afrika pia ni benki iliyo katika mwelekeo wa kuwa benki pendwa kwa wateja.

Soma na hizi

Tupia Comments