Makumi kwa maelfu ya wakimbizi wa Sudan, wengi wao wakiwa watoto, ambao wamevuka mpaka na kuingia Chad wako katika hatari ya “maafa makubwa ya kibinadamu” wakati msimu wa mvua unapoanza ndani ya wiki, afisa wa Msalaba Mwekundu ameonya.
Takriban watu 80,000 wametafuta hifadhi katika nchi hiyo iliyoko magharibi mwa Sudan huku mapigano ya wiki kadhaa kati ya majenerali wawili wanaopigana yakiwalazimisha mamia kwa maelfu kuyahama makazi yao.
Lakini wakimbizi, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wanawasili kwa kasi kiasi kwamba shughuli za kibinadamu katika eneo hilo zitatatizika kuwahamisha wote hadi mahali pa usalama kabla ya mvua kunyesha mwishoni mwa mwezi wa Juni, na uwezekano wa kukata sehemu kubwa ya mpaka.
.
Aidha umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya misaada ya kibinadamu, imesema tayari pande hasimu zimetenganishwa na kwamba ndani ya saa chache zijazo baadhi ya misaada itaanza kuwafikia raia waliokuwa wamenasa katika mapigano.
Miongoni mwa mamia ya familia za wakimbizi waliokuwa wakingoja mpakani, baadhi yao hawakuwa na pasipoti.
Wengine hawangeenda mbali zaidi hadi mume wao, kaka au mwana wao apewe visa — ambayo wanawake na watoto hawaruhusiwi.
Tangu mapigano yalipoanza Aprili 15 kati ya vikosi vya majenerali wawili hasimu, zaidi ya wakimbizi 132,000 wamewasili Misri, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilisema Jumatano.
Zaidi ya wengine milioni moja wamekimbia makazi yao ndani ya Sudan, na kuvuka mipaka ya nchi zingine.
Wengi wa wale ambao hawakuweza kukimbia wamejificha majumbani mwao bila vifaa vya msingi.
Kwa wale wanaovuka mpaka hadi Misri, Msalaba Mwekundu wa Misri hutoa huduma kwa wagonjwa na hutoa maji na biskuti.
Kwa sasa hali ya utulivu imeshuhudiwa katika maeneo mengi ya nchi licha ya kuwa hapo jana kuliripotiwa mashambulio kadhaa ya anga kwenye mji wa Khartoum, ingawa nchi za Marekani na Saudi Arabia ambazo ndio wasimamizi wa mkataba huo wanasema hali ni tofauti na siku chache zilizopita.
Hata hivyo licha ya kuripotiwa kwa hali ya utulivu na makabiliano kidogo, wasimamizi wa mkataba huo wamezituhumu pande zote mbili kwa kukiuka sehemu ya makubaliano hayo, ambapo wameonya kuchukua hatua