AyoTV

VIDEO: Mambo matano kutoka Azam FC baada ya cheo cha CEO kufutwa

on

Jana June 1 2017 club ya Azam FC itangaza rasmi kumalizana na aliyekuwa afisa mtendaji Mkuu wa club hiyo  Saad Kawemba (CEO) kutokana na mkataba wake kumalizika, walitangaza kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa club na utawala lakini afisa habari wa club hiyo Jafari Idd kaongea na wanahabari leo.

1- Azam FC leo wametangaza rasmi kuachana na wachezaji Hamis Mcha na Ame Ally ambao wote mikataba yao imemalizika lakini Ame mkataba wakeume malizika akiwa Kagera Sugar kwa mkopo.

2- Ni kweli cheo cha CEO kimefutwa na cheo cha General Manager alichokuwa nacho Abdul Mohamed ndio kinakuwa cheo cha juu kwa maana ya mtendaji Mkuu wa club hiyo.

3- Azam FC imethibitisha kubadili falsafa ya usajili na kujikita zaidi kuwa timu itakuwa inapandisha wachezaji kutoka katika Academy yao na imeanza kwa kuwapandisha Abbas Kapombe, Ramadhani (Ramaninho), Yahaya Zaid, Staslaus Rwakatare, Abdul Haji, Godfrey Elias.

4- Rasmi Azam FC imetangaza kuachana na utaratibu wa kusajili wachezaji kwa kutumia fedha nyingi na kwa kiasi kikubwa imejikita kusajili wachezaji wa ndani ya Tanzania, Azam FC katika maandalizi ya msimu ujao hawataweka kambi nje ya nchi.

5- Afisa habari wa Azam FC Jafari Idd amekanusha na kuomba ieleweke kuwa hakuna matatizo au ugomvi wowote kati ya Genera Manager wa timu hiyo Abdul Mohamed na CEO wa zamani wa timu hiyo Saad Kawemba yanayoandikwa ni uzushi tu.

VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera

Soma na hizi

Tupia Comments