Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imezindua msimu wa kampeni ya kuhamasisha utalii kwa wananchi kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka yenye kauli mbiu isemayo _MERRY AND WILD, NGORONGORO AWAITS_ ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 4 Desemba, 2024 hadi tarehe 4 Januari, 2025.
Akitangaza kampeni hiyo Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Idara ya huduma za utalii na Masoko amesema watashirikiana na wadau mbalimbali ili kuwawezesha watanzania wengi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro.