Michezo

Louis van Gaal anaondoka Man United? imenifikia list ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi yake …

on

Headlines za makocha mbalimbali wa Ligi Kuu Uingereza kufukuzwa zinaendelea kushika kasi ambapo hivi karibuni ulimwengu ulishuhudia Kocha wa Swansea City Garry Monk akifukuzwa na Jose Mourinho akifukuzwa kuifundisha Chelsea.

Stori za mitandaoni za hivi karibuni ni zile zinazomzungumzia Kocha wa Manchester United Louis van Gaal na hatma yake ndani ya klabu hiyo baada ya timu yake kuendelea kufanya vibaya, hivyo kumekuwa na list ya makocha wengine wanaotajwa kurithi nafasi yake mtu wangu.

Kupitia mtandao wa ‘The Telegraph’ pamoja na taarifa zilizopo ndani ya Manchester United zinatajwa, Kocha aliyefukuzwa kuifundisha Chelsea, Jose Mourinho yupo kwenye list ya makocha wanaotajwa kumrithi Van Gaal Man United. Mourinho alifukuzwa na Chelsea baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo mbovu.

José-Mourinho

Jose Mourinho

Kocha mwingine anayetajwa ni Pep Guardiola ambaye anaifundisha klabu ya Bayern Munich inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani, kwani hivi karibuni alikataa kuongeza mkataba wa kuendelea kuifundisha  FC Bayern Munich. Mkataba wa Gurdiola ndani ya Bayern unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.

_78365113_pep_guardiola_getty3

Pep Guardiola

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments