Michezo

Man City wanatinga fainali ya UEFA, msimu huu wameamua

on

Club ya Man City leo ikiikaribisha PSG katika uwanja wao wa Etihad kucheza mchezo wao wa pili wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya ule wa awali uliyopigwa wiki moja nyuma Man City kushinda 2-1.

Leo Man City wakiwa nyumbani kupitia kwa staa wao Riyad Mahrez wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli yote yakofungwa na Mahrez dakika ya 11 na 63, hivyo Man City wanatinga fainali ya UEFA.

Man City hii ni mara yao ya kwanza kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Kocja wao Pep Guardiola akifika hatua hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10, Man City watacheza fainali na mshindi wa mechi ya kesho kati ya Chelsea vs Real Madrid.

Soma na hizi

Tupia Comments