Club ya Man City ya Ligi Kuu England imeingia matatizoni baada ya Ligi Kuu England kuwashitaki kwa tuhuma za kukiuka kanuni na sheria za matumizi ya pesa (Financial Fair Play).
Makosa ya Man City yanadaiwa kufanyika kwa miaka 9 kuanzia 2009/2010-2017/2018, baada ya uchunguzi kufanyika kwa miaka minne sasa wanaweza kukumbana na adhabu ya kukatwa point.
Suala la kama hili hivi karibuni limeigharimu club ya Juventus ya Italia ambayo ilikatwa point 15 kwa madai ya kukiuka sheria za matumizi Italia.