Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Mikakati ya Manchester United kwa mshambuliaji huyu wa Uholanzi!!

on

mem

Dirisha la usajili wa ligi kuu ya England bado halijafunguliwa rasmi na linatarajiwa kufunguliwa mwezi ujao kupisha timu kusajili wachezaji watakaoongeza nguvu ndani ya vikosi vyao.

Ikiwa katika harakati za kujiwekea mikakati ya kufanya vizuri msimu ujao, Manchester united ambayo inawania nafasi ya timu tatu bora kwenye ligi kuu imetangaza kumsajili mshambuliaji wa klabu ya PSV, Memphis Depay kwa ajili ya msimu ujao.

Manchester United imetenga dau la pauni milioni 25-30 ili kumpata nyota huyo ambaye atadumu ndani ya kikosi hicho hadi 2019.

Depay ambaye aliisaidia timu yake kufunga mabao 21 msimu huu, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya wiki ijayo na atajiunga na klabu hiyo baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments