Mabosi wa Manchester United wamefanya mazungumzo na timu mbalimbali barani Ulaya ikiwamo Real Betis, kwa ajili ya kumuuza winga wao raia wa Brazil, Antony katika dirisha hili.
Man United inataka kumuuza Antony mwenye umri wa miaka 24, ili kupunguza gharama za uendeshaji timu kwa sababu hayupo katika mipango ya kocha Ruben Amorim na anachukua mshahara mnono.
Antony aliyesajiliwa mwaka 2022 kwa ada ya Euro 95 milioni akitokea Ajax, anakunja mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki akiwa mmoja kati ya mastaa wanaolipwa zaidi kwenye timu hiyo.
Msimu huu amecheza mechi 12 za michuano yote na kufunga bao moja na mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.
Hata hivyo, wakala wa staa huyu amekuwa akisisitiza kwamba mchezaji wake haendi kokote na anataka kupambania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza.
2 hSee Translation