Club ya Man United imetangaza kuachana na staa wake Cristiano Ronaldo (37) kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Man United imemshukuru Ronaldo kwa utumishi wake wa vipindi viwili tofauti katika club hiyo “Cristiano Ronaldo anaondoka Man U kwa makubaliano ya pande zote mbili, club inamshukuru kwa mchango wake wa vipindi viwili Old Trafford (2003-2009 & 2021-2022).
Mkataba wa Ronaldo na Man United ulikuwa unaisha mwisho wa msimu 2022/23 lakini inawezekana mahusiano yake mabovu na Kocha Erik Ten Hagen pamoja na interview yake na Piers Morgan vimechochea mkataba huo kuvunjika.