Manchester United wamepanga kuuzwa kwa Jadon Sancho kwa pauni milioni 40 na wamedhamiria kumuondoa bila kujali meneja wao ni nani msimu ujao, linaripoti The Sun.
Winga huyo mwenye thamani ya pauni milioni 73 alizuiwa na bosi wa United Erik ten Hag mwezi Agosti baada ya kutofautiana na Mholanzi huyo na kukaa uhamishoni kwa miezi minne kabla ya kupelekwa kwa mkopo kwa klabu yake ya zamani Borussia Dortmund mwezi Januari.
Sancho alifanya vyema nchini Ujerumani na kuwasaidia kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Wembley mapema mwezi huu, jambo ambalo liliibua matarajio kuwa bado anaweza kuwa Old Trafford – hasa ikiwa Ten Hag ataondolewa majukumu yake.
Hata hivyo, ripoti inasema United wameweka wazi kuwa wangependelea kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 – na wameweka bei kwa klabu zozote zinazomtaka.