Michezo

Hii ni ya shabiki wa Manchester United aliepiga simu polisi

on

 

man-u-fan

Mlevi mmoja huko Uingereza ambae ni shabiki wa Manchester United amepiga simu 999 akiagiza kwamba anataka kuongea na kocha aliepita ambae ni Sir Alex Ferguson kuhusu matokeo ya mechi baada ya club hii kutolewa Capital One cup.

Huyu shabiki akiwa na uchungu aliwapigia simu polisi ambao wapo kaskazini mwa mji huo muda mfupi tu baada ya Red Devil’s kushindwa na kutolewa na Sunderland kwa mikwaju.

Polisi wa Greater Manchester walitoa tamko wakisema “Jana usiku saa nne na nusu mwanaume mmoja kutoka maeneo ya Crumpsall kaskazini mwa Manchester alipiga simu 999 akiwa na sauti ya mtu aliyelewa akiamuru koungea na Sir Alex kuhusu matokeo ya mechi, ni kawaida kuwa na machungu pale timu yako inaposhindwa lakini tukumbuke namba 999 ni kwa ajili ya huduma za dharura tu kwa raia ndio maana kwa visivyo vya dharura namba 101 ndio inatumika’

Screen-Shot-2014-01-24-at-2.33.09-AM

 

Taarifa ya polisi kwenye sentensi hii imesema ‘kama mtu angependa kuzungumza na Sir Alex kuhusu matokeo ya mechi sisi GMP Manchester Kaskazini tunakushauri upige simu Manchester FC kwakuwa unaweza ukawa na bahati zaidi ya kumpata huko kuliko kupiga simu polisi.

Tupia Comments