Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ameiambia klabu hiyo kuwa anataka kuondoka kutafuta maisha mengine, huku Manchester City ikiwa ni timu pekee inayoonyesha shauku ya kutaka kumsajili.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Esporte Interativo’ wa Hispania Messi 33, anashinikiza kuondoka kutokana na matokeo mabaya yanayoikumbu timu.
Barcelona ilikula kichapo cha mabao 8-2 kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka kwa Bayern Munchen.