Napoli inasemekana kua wapo tayari kumtoa Victor Osmihen kwa Manchester United ili kuwaweka pembeni katika mazungumzo ya kumsajili Alejandro Garnacho.
FF TV inadai kwamba mapendekezo ya Garnacho kwenda Napoli yanazidi kushika kasi, lakini timu hiyo ya Italia ina wasiwasi na Chelsea.
United wanataka angalau pauni milioni 50 kwa nyota wao chipukizi wa Argentina lakini Napoli wametoa karibu pauni milioni 15 pamoja na Osimhen, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray.
La Repubblica inasema United sasa wamewasilisha ofa ya pesa taslimu €100m kwa Osimhen.
Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis ana mpango huo mbele yake na leo anapanga kukutana na maajenti wa mchezaji huyo kujadili uhamisho huo.
Kwa upande wake, Osimhen ana matarajio ya kucheza Ligi ya Premia, ingawa ukosefu wa United kwenye Ligi ya Mabingwa inaweza kuwa suala.
Mshambuliaji huyo amefunga mabao 16 katika mechi 28 msimu huu, baada ya kujiunga na Napoli mwaka 2020 kutoka Lille kwa €75m.