Michezo

Baada ya Man City Roberto Mancini ameangukia wapi time hii?

on

ManciniUnaambiwa kwenye maisha hautakiwi kuwafanyia chochote kiubaya Watu unaokutana nao maishani au kumfanyia yeyote ubaya sababu hujui kesho na keshokutwa utakua wapi…… inawezekana Roberto Mancini aliifata hii kanuni na ndio maana amerudi kufanya kazi kwenye sehemu ambayo aliifanyia kazi kuanzia 2004 mpaka 2008.

Kocha huyu alieifundisha Manchester City kuanzia 2008 -2013 ametangazwa kuchukua nafasi ya kocha Walter Mazzarri aliyetimuliwa na Club ya Inter Milan Ijumaa ya November 14 2014 na sasa nafasi yake inachukuliwa na Mancini.

RaisInasemekana maamuzi ya kumtimua Mazzarri yalifikiwa ndani ya usiku mmoja na Rais wa Inter Milan Erick Thohir ambae tayari alikua amemuweka Mancini akilini na inaaminika kocha huyu amepewa mkataba wa miaka miwili na nusu.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments