Michezo

Eti ni kweli wachezaji wa Man City wameamua kuchagua kocha wao mpya ??

on

Manchester-City

Kibarua cha kocha raia wa Chile Manuel Pelegrini ndani ya klabu ya Manchester City kinaendelea kuwa hatarini hasa katika kipindi hiki ambacho klabu hii imekuwa ikipata matokeo yasiyoridhisha.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani wamiliki wa klabu hii wanajindaa kumuonesha kocha huyo  mlango wa kutokea huku chaguo la wakurugenzi wa timu hiyo likiwa Mhispania Pep Guardiola ambaye kwa sasa yuko Bayern Munich.

Hata hivyo wachezaji wa timu hiyo kwa upande mwingine wamekuwa na mtazamo tofauti ambapo inasemekana kuwa endapo Pelegrini atafukuzwa chaguo lao ni kiungo wa zamani wa klabu hiyo Patrick Vieira.

Mpango uliopo miongoni mwa Mkurugenzi Mtendaji Feran Soriano na Txiki Berigistan ambaye ni mkurugenzi wa michezo ni kungoja mkataba wa Pelegrini umalizike na kumuajiri Guardiola ambaye wakati huo atakuwa amemaliza mkataba wake na Bayern.

Kiungo wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira ametajwa kuwa chaguo la wachezaji wa Man City kama kocha endapo Manuel Pelegrini atafukuzwa.

Kiungo wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira ametajwa kuwa chaguo la wachezaji wa Man City kama kocha kama ikitokea kibarua cha Manuel Pelegrini kitaota nyasi.

Hata hivyo kama City itashawishika kumfukuza kocha wake wa sasa baada ya msimu huu kumalizika wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza cha Man City wangependa kumuona Patrick Vieira akipewa nafasi kama kocha mkuu wa klabu hiyo kutokana na heshima waliyo nayo kwake.

Vieira ambaye anakumbukwa zaidi akiwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kilichokuwa na mafanikio kuliko hata mwaka mmoja aliocheza Man City amekuwa kocha na mkurugenzi wa timu za vijana za Man City na amekuwa akisomea ukocha kwa muda wake wa ziada huku akingoja nafasi yake katika klabu kubwa.

Mhispania Pep Guardiola ndio chaguo la kwanza la wakurugenzi wa Man City kurithi nafasi ya Manuel Pelegrini.

Mhispania Pep Guardiola ndio chaguo la kwanza la wakurugenzi wa Man City kurithi nafasi ya Manuel Pelegrini.

Patrick Vieira alichezea Manchester City kwa kipindi cha msimu mmoja baada ya kusajiliwa na Roberto Mancini akitokea Inter Milan na alicheza na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Man City kama Jo Hart na Vincent Kompany.

Tupia Comments