Michezo

Man Utd vs Man city… ni mara ya ngapi kukutana leo? rekodi nyingine je?

on

ad_116403401Wapinzani wa jiji la Manchester kwenye soka Manchester United na Manchester City wanakutana leo katika mechi ya raundi ya ligi kuu ya England kwenye uwanja wa Old Trafford.

Wakati tunaisubiria hii mechi hizi ni baadhi ya takwimu kutoka hapa millardayo.com ambapo unaambiwa hii ni mechi ya 150 katika historia ya upinzani wa club hizi lakini pia Manchester Utd wamepoteza mechi zote nne za north west derbies katika Premier League msimu huu.

*Man City hawajafungwa katika mechi zao 8 zilizopita ugenini na wameshinda sita na kutoa sare 2, vilevile wameshinda mechi 4 katika ya 5 zilizopita dhidi ya Manchester United zikiwemo mbili walizocheza Old Trafford.

*Manchester United hawajashinda katika mechi 2 zilizopita za Premier League walizocheza katika uwanja wa nyumbani ambapo katika mechi zote walizocheza na timu sita za juu kwenye msimamo wa ligi, United wameshinda mara 1 tu dhidi ya Arsenal msimu huu.

*Wayne Rooney amefunga magoli yote matano katika mechi tano zilizopita dhidi ya Manchester City ambapo City hawajaruhusu wavu wao kuguswa katika premier league ndani ya dakika 418.

Tupia Comments