Ni June 1, 2023 ambapo sehemu mbambali inaadhimisha siku ya Maziwa Duniani.
Sasa hapa tunae Mkurugenzi wa kampuni ya Asas inayohusika kusambaa na uuzaji wa Maziwa Tanzania, Ahmed ambae ametuma salamu kwa watanzania hususani katika siku hii ya leo ya maadhimisho hayo.
“Kuna umuhimu sana wa unywaji wa maziwa kwa watu kwani kitaalamu kwa mujibu wa Shirika la afya duniani ( WHO) wanasema binadamu anapaswa anywe maziwa walau lita 200 kwa mwaka”- Ahmed Asas
“Kiutaalamu wanashauri maziwa bora ni yale yaliyosindikwa na usindikaji sio kutumia kemikali,maziwa yetu yanachemshwa kuwekwa katika vifungashio vizuri na kuongezewa radha,”amesema
‘Na ikiwa leo ni siku ya Maziwa Duniani nashauri kwa kila mtanzania kuhakikisha anakunywa hata glasi moja ya maziwa ya Asas ili aungane na mataifa mbalimbali katika kuadhimisha siku hii ya leo”- Ahmed Asas
“Maziwa yetu ni mazuri sana kwa afya na virutubisho vinavyopatikana vinaongeza virutubisho ambavyo mwili vinahitaji tunashauri kila mtanzania anywe maziwa walau hata lita moja kwa siku,”amesema