Top Stories

Maneno ya Mwisho ya Malcom kwa mama yake “Mama nakufa tafuta mtoto”(video+)

on

Ikiwa bado tuko kwenye Simanzi na Majonzi baada ya kufariki kwa mtoto wa Mtangazaji Masoud Kipanya aitwae Malcom Ally.

Sasa hapa tumempata mtangazaji aitwae Bonge kutoka Radio Clouds FM akieleza marehemu Malcom akieleza kauli za mwisho za Marehemu Malcom

“Dakika za mwisho Dereva wa Ambulance anasema Malcom wakati wanarudi nae nyumbani alikuwa sawa na  Mama yake alituambia kwamba alisema Malcom alikuwa akimwambia kuwa anakufa na siku kadhaa zilizopita Malcom aliwahi kumwambia Mama yake kwambia itabidi atafuta mtoto mwingine kwani akifariki yeye atabaki na nani?”- Bonge wa Power Breakfast

“Kwahiyo Malcom kama aliziona siku zake za mwisho kwani Mama yake alikuwa ananiambia kwamba Bonge unajua Malcom alikuwa ananiaga basi mimi nikawa namwambia kazi ya Mola haina makosa”- Bonge wa Power Breakfast

“Malcom  shida yake kubwa ilikuwa ni kutokukua kwa Misuli unaona watu wanamshangaa ana chart kwenye simu hivi lakini kusogeza kitu hawezi na ndio kilichosababisha kulala kitandani zaidi ya miaka 10′- Bonge

DEREVA ALIENDESHA MWILI WA MALCOM ASIMULIA ALIVYOMFAHAMU

Soma na hizi

Tupia Comments